MWANARIADHA WA KENYA AFARIKI KWA AJALI YA GARI


Nicholas Bett, akifurahia ushindi katika mbio za mashindano ya World Championship 2015

Mwanariadha wa Kenya, Nicholas Bett, amefariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea leo asubuhi katika barabara ya Eldoret na Kampsabet, nchini Kenya

Kwa mujibu wa Kocha wake, Vicent Mumo, Bett alifariki baada ya gari alilokuwa akisafiria kugonga tuta katika barabara yenye miinuko na kuanza kuserereka majira ya saa 12 asubuhi,

Bett (28), aliwahi kuwa bingwa wa dunia na kushinda medali ya dhahabu mwaka 2015 katika mashindano ya World Championship Beijing.

Mwaka 2014, Marehemu Bett alijinyakulia medali mbili za shaba kwenye African Championship yaliyofanyika Morocco. Medali hizo zilikuwa katika mbio za kuruka viunzi (400m) na mbio za kupokezana na wenzake (4x400m).

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametoa pole kwa wakenya, ndugu, jamaa na marafiki wa familia ya mwanariadha huyo kupitia mtandao wa Twitter huku akisifia uwezo wake na kuwa aliipa nchi yake heshima.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.