NHIF KAGERA YAHAMASISHA USHIRIKA AFYA KWENYE MAONYESHO YA NANE NANE.


Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akipima afya kwenye banda la mfuko wa bima ya afya(NHIF)kwenye viwanja vya Kyakailabwa wakati wa sherehe za nane nane - Picha na Editha Karlo - Malunde1 blog Kagera
***

MFUKO  wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Kagera umewahamasisha wakulima kupitia vyama vya ushirika na masoko kujiunga na mpango wa ushirika afya (AMCOS)katika maonesho ya nane nane Mkoani humu yalifonyika katika viwanja vya Kakyailabwa (AMCOS)Kujiunga na mpango wa ushirika afya viwanja  Kyakailabwa.

Akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Maico Gaguti  Meneja wa Mfuko wa bima ya afya Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo alisema kuwa ushirika afya ni mpango maalum wa Bima ya afya kwa wakulima ambapo mpango huo utawawezesha wakulima kuchangia mara moja gharama za matibabu na kuwa na uhakika wa matibabu kwa mwaka mzima pale wanapougua.

Odhiambo alisema  watakaojiunga na mpango huu watapata matibabu kwenye vituo vya tiba vilivyosajiliwa na mfuko nchi nzima ikiwa ni pamoja na huduma za kibingwa na vipimo.

Katika viwanja vya kyakailabwa kwenye maonyesho ya sikukuu ya nane nane  banda la NHIF lilisheheni huduma mbali mbali ikiwa ni pamoja na upimaji afya bila malipo kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza, usajili wa Ushirika Afya,Toto Afya na Bima kwa wajasiliamali.

Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Generali Marco Gaguti alitembelea banda la NHIF na kushiriki katika upimaji wa Afya pia alihaidi kuhamasisha wakulima kujiunga na mpango huo kwaninutawasaidia wakulima kuwa na  uhakika wa matibabu pale wanapougua wao na familia zao.

Na Editha Karlo - Malunde1 blog Kagera
Meneja wa Bima ya afya Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Maico Gaguti juu ya mpango wa ushirika afya kwa wakulima
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti akipata maelezo kutoka kwa mtumishi wa mfuko wa bima ya afya katika banda la NHIF baada ya kutembelea kwenye nane nane katika viwanja vya Kyakailabwa
Wananchi wakipata maelezo mbalimbali katika banda la mfuko wa bima ya afya(NHIF)Mkoa wa Kagera katika viwanja vya kyakailabwa maonyesho ya nane nane. Picha na Editha Karlo - Malunde1 blog Kagera

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527