DIWANI WA CHADEMA AHAMIA CCM BAADA YA KUVUTIWA NA DREAMLINER

Uamuzi mgumu wa Rais John Magufuli wa kuboresha usafiri wa anga nchini kwa kununua ndege kubwa ya Boeing 787-8 Dreamliner, umemkimbiza Diwani wa Chadema katika kata ya Ndumeti, Wilaya ya Siha, Jackson Rabo kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kwa mujibu wa diwani huyo moja ya sababu iliyomvutia kujiunga na CCM baada ya uamuzi wa Rais John Magufuli kuhamishia ofisi zote za serikali mkoani Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Valerian Juwal amethibitisha kuwa Diwani Jackson Rabo anakuwa Diwani wa tano katika wilaya hiyo kujiuzulu mwaka huu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527