Wednesday, July 11, 2018

WIZARA YA VIWANDA NA AFYA WAPOKEA WAWEKEZAJI WA SEKTA YA AFYA KUTOKA CHINA

  Malunde       Wednesday, July 11, 2018

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Bwana Laurean Bwanakunu Rugambwa (kulia), akiwa na viongozi wenzake kutoka Wizara ya ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dar es Salaam leo wakati wakiupokea ujumbe wa wawekezaji wa sekta ya Afya kutoka kampuni ya Kimataifa ya Fosun kutoka China, ambao wamekuja kuwekeza kwenye viwanda vya uzalishaji dawa na vifaa tiba. 
Mkutano na wawekezaji hao ukiendelea. 
Mkutano ukiendelea. Katikati kulia ni Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na Waziri wa Viwanda, Charles Mwijage.
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage (wa nne kutoka kushoto) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe huo kutoka China. Wa tatu kutoka kushoto ni Rais wa Fosun Pharma,Willium Yifang WU.


Na Dotto Mwaibale

WIZARA ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji kwa kushirikiana na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto wamepokea ujumbe wa wawekezaji wa sekta ya Afya kutoka kampuni ya Kimataifa ya Fosun kutoka China, ambao wamekuja kuwekeza kwenye viwanda vya uzalishaji dawa na vifaa tiba. 


Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage (Mb.) ameeleza kuwa msimamo wa serikali ni kuhakikisha viwanda vinajengwa nchini ili kupunguza mzigo wa kununua dawa nje ya nchi kwa gharama kubwa,kupoteza ajira na pato la serikali.


Kwa upande wake,Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu amesema asilimia 94 ya fedha za bajeti zinazotengwa kwa ajili ya kununua dawa,vifaa tiba na vitendanishi vya maabara hupelekwa nje ya nchi,na asilimia 6 tu ndio hununua kutoka viwanda vya ndani.Hii ni kwa sababu hakuna viwanda vinavyoweza kuzalisha dawa tunazozihitaji.


Wataalamu walioshiriki majadiliano na wawekezaji hao ni pamoja na Bohari ya Dawa(MSD),Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA),Kituo cha Uwekezaji nchini(TIC),Mamlaka ya Uwekezaji(EPZ) na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC).


Rais wa Fosun Pharma,Willium Yifang WU amesema ili wawekeze wanahitaji ardhi ekari 10 kwa ajili ya kuanzisha kiwanda.


Kwa mujibu wa Waziri Mwijage wawekezaji hao wakiwa tayari serikali itawapatia eneo kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho cha dawa.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post