CROATIA WAINYUKA DENMARK - KUKWATUANA NA URUSI ROBO FAINALI JULAI 7


Wachezaji wa Croatia wakishangilia bao lao la kusawazisha dhidi ya Denmark.

Timu ya taifa ya Croatia imefanikiwa kutinga hatua ya robo Fainali ya Kombe la Dunia baada ya kushinda kwa penati 3-2 dhidi ya Denmark baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya 1-1. 


Ushindi huo wa Croatia umeifanya nchi hiyo kuvunja mwiko ambao umedumu kwa miaka 20 wa kufuzu hatua ya robo fainali ambapo mara ya mwisho ilifika hatua hiyo ilikuwa ni kwenye Fainali zilizofanyika mwaka 1998 nchini Ufaransa.

Croatia ilitokea nyuma na kusawazisha dakika ya 4 bao lililofungwa sekunde ya 57 tu na Mathias Jørgensen wa Denmark. Mshambuliaji Mario Mandzukic ndio alisawazisha ambapo mchezo ulidumu kwa 1-1 hadi dakika 120 na baadae penati.

Katika mikwaju ya penati Denmark walikosa tatu na kupata 2 huku Croatia wakikosa mbili na kupata 3. Waliokosa kwa upande wa Denmark ni nahodha Christian Eriksen, Lasse Schøne na Nicolai Jørgensen. Kwa Croatia wamekosa Milan Badelj na Josip Pivaric.

Waliopata kwa upande wa Denmark ni Simon Kjær na Michael Krohn-Dehli. Croatia waliopata ni Andrej Kramaric, Luka Modric na Ivan Rakitic. Timu hiyo sasa itakutana na wenyeji wa Fainali hizo timu ya Urusi kwenye mchezo wa robo fainali.


Theme images by rion819. Powered by Blogger.