Tuesday, July 3, 2018

IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA POLISI TANZANIA

  Malunde       Tuesday, July 3, 2018

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amefanya mabadiliko ya makamanda wa polisi kwa baadhi ya mikoa.


Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Julai 3, 2018 iliyosainiwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa, inasema mabadiliko hayo yanalenga kuongeza juhudi za kuzuia ajali zilizotokea mara kwa mara katika baadhi ya mikoa.

Katika mabadiliko hayo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Deusdedit Nsimeki aliyekuwa makao makuu ya upelelezi Dar es Salaam anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi (RPC) Mkoa wa Simiyu.

Aliyekuwa RPC Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ulrich Matei anakwenda kuwa RPC Mkoa wa Mbeya.

Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kaimu RPC Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi, Mussa Taibu amehamishiwa makao makuu ya polisi Dar es Salaam.

Aliyekuwa RPC Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Wilbroad Mutafungwa anakwenda kuwa RPC Mkoa wa Morogoro, nafasi yake ikichukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi, Emmanuel Nley kutoka makao makuu ya polisi Dar es Salaam.

Wengine waliohusika na mabadiliko hayo ni aliyekuwa Ofisa Mnadhimu Mkoa wa Geita Kamishna Msaidizi wa Polisi, Stanley Kulyamo anayekwenda kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Tazara.

IGP Sirro amewataka makamanda wa polisi wa mikoa nchini, kuendelea kuwajibika ipasavyo katika kuhakikisha ajali hazitokei katika maeneo yao na kuwachukulia hatua kali madereva watakaosababisha ajali kwa uzembe.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post