Tuesday, July 3, 2018

USWIZI NJE YA KOMBE LA DUNIA...SWEDEN NDANI YA ROBO FAINALI

  Malunde       Tuesday, July 3, 2018

Wachezaji wa Sweden wakishangilia baada ya kufunga bao lililowapeleka robo fainali.

Timu ya taifa ya Sweden imeibuka na ushindi wa bao 1-0, kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora Kombe la Dunia dhidi ya Uswizi (Switzerland) iliyomalizika usiku wa Julai 3,2018 huko Saint Petersburg huko Urusi.

Ushindi huo wa Sweden umeichukua historia ya Kombe la Dunia na kuirudisha nyuma hadi mwaka 1958, ambapo Sweden walikuwa wenyeji na walishinda mechi mbili mfululizo kwa mara ya kwanza robo fainali na nusu fainali na kutinga fainali.

Kabla ya kushinda dhidi ya Switzerland leo, Sweden ilitoka kushinda 3-0 mechi ya mwisho hatua ya makundi kwenye kundi F dhidi ya Mexico, hivyo mechi ya leo imekuwa ya pili mfululizo kwa Sweden kushinda.

Bao la Sweden limefungwa na kiungo Emil Forsberg ambaye mapema leo ripoti zilieleza kuwa kocha wa Manchester United Jose Mourinho, alitarajiwa kuwepo uwanjani kwaajili ya kumfuatilia nyota huyo ambaye ameibuka kiungo bora wa Sweden katika miaka ya 2014, 2016 na 2017.

Sweden ambayo leo imecheza mechi yake ya 50 kwenye Kombe la Dunia na kuwa timu ya pili kucheza mechi nyingi bila kuchukua ubingwa, sasa inasubiri mshindi kati ya England na Colombia ili kucheza naye katika hatua ya robo fainali.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post