SERIKALI YAWABANA WEZI WA DAWA

Serikali imeanzisha mfumo mpya wa kuweka nembo kwenye dawa zinazosambazwa na Bohari ya Dawa (MSD), ili kudhibiti wizi wa dawa za serikali unaofanywa na watumishi wake katika zahanati, vituo vya afya na hospitali.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile, alibainisha hayo katika ziara yake mkoani Mwanza, alipokuwa akikagua bohari za dawa na wodi za wagonjwa katika Hospitali ya DDH wilayani Sengerema.

Serikali tumeanzisha mfumo mpya wa kuweka nembo kwenye dawa zetu ambayo ni (GOT), ili kudhibiti wizi wa dawa za wagonjwa kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali unaofanywa na watumishi wake,” alisema Dk. Ndungulile.

“Serikali tumeanzisha mfumo huo mpya wa kuweka nembo kwenye dawa za tembe na makopo ili kuzuia kuibiwa na kuuzwa katika maduka ya dawa yakiwamo ya watumishi,” alisema zaidi Dk. Ndungulile.

Alisema kama mtu yeyote atabainika akiuza dawa zenye nembo hiyo awe mtumishi wa serikali au binafsi, atakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Akiwa Wilaya ya Sengerema, Naibu Waziri huyo alikagua zahanati ya kijiji cha Nyamizeze na kutoa zawadi ya cheti kutokana ubora wa huduma kwa kuwa na nyota nne.

Zahanati hiyo ilianzishwa mwaka 1964 na ina watumishi sita. Inahudumia vijiji vitatu vyenye wakazi 8,000 wanaotegemea kupata huduma kwenye zahanati hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527