EDO KUMWEMBE AWACHANA YANGA: “PESA SIO MAKALIO, TUJIFUNZE KUHESHIMU WENYE PESA”

Kinacho Trend katika mitandao ya kijamii kwa sasa ni suala la viongozi wa club ya Yanga kujiuzulu nafasi zao za uongozi ndani ya Yanga na kuiacha timu katika kipindi kigumu, hivyo sintofahamu inazidi kutanda nini itakuwa hatma ya timu hiyo kuelekea msimu wa 2018/19.
 
Kutokana na matatizo na changamoto zinazoendelea katika club hiyo mchambuzi wa masuala ya soka Edo Kumwembe ameandika maneno au ushauri katika ukurasa wake wa instagram ikilenga kuwakosoa wale mashabiki wa soka ambao wanapenda kuwakwaza wafadhili wa timu hizo.
 
“Pesa sio makalio kwamba kila mtu anayo……tujifunze kuheshimu watu wenye pesa..zile kelele za nyakati zile za watu fulani dhidi ya Manji..wakimpinga sana…wengine wakasema “Atuachie Yanga yetu”
 
“Leo ndo muda wao wa kuichukua Yanga yao, wakalipe Kambi, wawalipe akina Yondan na Kessy, washushe akina Kagere wao pale Jangwani Yaani Manji hayupo na hakuna atakayewakataza…yuko wapi yule Mzee? Yuko wapi yule kijana machachari?”
 
“Iliwahi kutokea pale Tanga..watu walimwambia Nassor Binslum awaachie timu yako..wakaishia kushuka na kupoteza dira…Simba iko Uturuki na kuna watu hawamtaki Mo..waambie wamsajili mchezaji mmoja tu kwa shilingi milioni kumi”
 
“Baada ya dakika tano ukiwapigia simu utasikia ‘Namba unayopiga haipatikani’…Pesa sio makalio kwamba kila mtu anayo…nadhani baada ya Yale yanayotokea Jangwani tutaanza kuheshimu wenye pesa…huu sio mpira wa nyakati za Ujamaa kwamba unamnunua Makumbi Juma kwa kumpa feni ya ukutani…tuheshimu wenye pesa!!! Asanteni”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527