MBUNGE AVULIWA UDIWANI KWA KUTOHUDHURIA VIKAO

Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Daudi Mayeji ametangaza Kata ya Ngamiani Kusini kuwa wazi kutokana na Diwani wake ambaye pia ni Mbunge wa Tanga Mjini, Mussa Mbaruku (CUF), kutohudhuria vikao zaidi ya sita vya Baraza la Madiwani.


Mayeji amesema mbunge huyo amepoteza sifa kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka za Majiji.


“Sheria ya Serikali za Mitaa, Mamlaka ya Majiji Sura ya 228, kifungu cha 30B ndiyo imemuondoa, ni kwa mujibu wa sheria,” amesema Mayeji.


Mbaruku aligombea nafasi hizo za ubunge na udiwani katika chaguzi Mkuu mwaka 2015, kupitia Chama cha Wananchi (CUF) na kushinda zote.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.