RONALDO AWEKA REKODI NYINGINE KUBWA JUVENTUS


Cristiano Ronaldo kwenye utambulisho wake ndani ya Juventus.

Christiano Ronaldo ameweka rekodi nyingine kubwa kwenye siku ya kwanza ya utambulisho katika klabu yake mpya ya Juventus ya Italia.

Katika utambulisho rasmi uliotanguliwa na vipimo vya Afya ambao uliofanyika Jumatatu, Julai 16, Ronaldo aliweka historia kwa klabu hiyo ya kuwa mchezaji aliyeuza jezi nyingi kwa siku moja baada ya klabu kuuza jezi 520,000 ambazo zimeiingizia klabu kiasi cha dolla millioni 60 zaidi ya shilingi billioni 136.

Idadi hiyo ya jezi ya Ronaldo iliyouzwa ni pungufu ya jezi 330,000 kuweza kuifikia idadi ya mauzo ya jezi ya msimu mzima wa 2016/17 ya mabingwa hao wa Italia.

“Najiona niko imara, kwangu hii ni changamoto nyingine. Ligi ni ngumu lakini kwakuwa Juventus wako tayari, na mimi nitakuwa tayari. Umri wangu si kitu muhimu, najiskia vizuri na niko tayari kwa kuianza kazi “. Alisema Ronaldo katika utambulisho wake.

Baadhi ya mashabiki wa Juventus wakionesha jezi ya Ronaldo.

Ronaldo alisajiliwa na klabu ya Juventus wiki iliyopita kwa dau la £105 milioni ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 317 kutoka Real Madrid kwa mkataba wa miaka minne, mkataba ambao utamfanya kuingiza kiasi cha Euro millioni 30 kwa mwaka.

Ujio wa Ronaldo katika klabu ya Juventus umeongeza umaarufu wa klabu na ligi ya Serie A, duniani ambapo baada tu ya Juventus kuthibitisha usajili wake iliongeza wafuasi wa mitandao ya kijamii zaidi ya million 1.5.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527