RAIS MAGUFULI AMTEUA KIHAMIA KUWA MKURUGENZI TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI - NEC...ANGALIA WOTE WALIOTEULIWA HAPA | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, July 1, 2018

RAIS MAGUFULI AMTEUA KIHAMIA KUWA MKURUGENZI TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI - NEC...ANGALIA WOTE WALIOTEULIWA HAPA

  Malunde       Sunday, July 1, 2018


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amefanya uteuzi wa mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), pamoja na makamishna watatu wa tume hiyo.


Rais Magufuli amefanya mabadiliko hayo leo, kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Balozi John Willium Kijazi, ambayo imesema kuwa Rais amemteua Athumani Kihamia kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kuchukua nafasi iliyoachwa na Ramadhani Kailima ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani.

Kabla ya uteauzi huo Kihamia alikuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, aidha Rais amefanya uteuzi pia wa makamishna wa tume ya uchaguzi, ambao ni Mbaruk Salim anayekuwa makamu mwenyekiti wa tume, Jaji mstaafu Thomas Mihayo na Balozi Omary Mapuli.

Balozi Kijazi amesema kuwa baada ya uteuzi wa viongozi hao, taarifa kuhusu tarehe ya kuapishwa itatolewa hivi karibuni.
.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post