Breaking : RAIS MAGUFULI AMTUMBUA MWIGULU NCHEMBA... KANGI LUGOLA ACHUKUA NAFASI

                                   Mwigulu Nchemba

Kangi Lugola

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika baraza lake la Mawaziri, ambapo amemteua (Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira), Kangi Lugola kuwa waziri wa Mambo ya ndani ya nchi kuchukua nafasi nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Mwigulu Nchemba.

Rais Magufuli amefanya mabadiliko hayo leo mchana Jumapili Julai 1,2018  kupitia Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Balozi John Willium Kijazi.

Taarifa hiyo imesema kwamba nafasi ya Kangi Lugola, inaenda kuchukuliwa na Mbunge wa Singida Mjini, Mh. Mussa Ramadhan Sima.

Aidha Rais amefanya uteuzi wa Naibu Waziri katika Wizara ya kilimo kutokana na umuhimu wa Wizara hiyo, ameongeza Naibu mwingine ambaye ni Mbunge wa Morogoro Kusini, Omary Mgumba.

Pamoja na hayo, katika mabadiliko hayo madogo, Rais Mgufuli amefanya Uhamisho Waziri Prof. Makame Mbarawa kutokea Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi anaenda kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, na aliyekuwa kwenye Wizara hiyo, Mhandisi Isack Kamwelwe anaenda kuwa Waziri wa Uchukuzi.

Hata hivyo Balozi Kijazi amesema tarehe ya kuapishwa kwa viongozi hao itatajwa hapo baadaye.

Theme images by rion819. Powered by Blogger.