Monday, July 30, 2018

DREAMLINER YATUA KWA MARA YA KWANZA KANDA YA ZIWA

  Malunde       Monday, July 30, 2018
Wakuu wa mikoa sita jana, walikuwa miongoni mwa wageni walioipokea ndege mpya aina ya Boeing 787-8 kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza.


Wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella wakuu wa mikoa walishuhudia ndege hiyo ya kisasa, ikitua kwa mara ya kwanza mjini hapa saa 4:19 asubuhi ikiwa na abiria 255.


Wakuu wa mikoa hiyo, Adam Malima (Mara), Mhandisi Robert Gabriel (Geita), Zainabu Telack (Shinyanga), Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu (Kagera) na na Anthony Mtaka (Simiyu) na viongozi dini


Akizungumza wakati wa mapokezi ya ndege hiyo,Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwele alisema Serikali ina mpango wa kuboresha majengo ya abiria na mizigo ikiwa ni pamoja na upanuzi wa viwanja vya ndege nchini.


Alisema baada ya kuanza upanuzi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,Uwanja wa Ndege wa Songwe, sasa wametenga fedha kwa ajili ya uwanja wa ndege wa Mwanza.


Alisema uwanja wa Mwanza ndiyo mrefu kuliko viwanja vyote, ukiwa na urefu wa kilomita 3.9, kubainisha kwamba ujio wa ndege mpya aina ya Boeing 787-8 (Dreamliner) utakuwa kichocheo kikubwa cha uchumi na maendeleo.


Naye Mongela alisema safari ya Mwanza kwenda Dar es Salaam kupitia Kilimanjaro kwa ndege, ni muhimu hivyo huduma ujio wa ndege ni muhimu sana kwa wakazi wa Mwanza na mikoa jirani.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post