VIFO NA MAISHA YA MAPACHA WA PEKEE MARIA NA CONSOLATA DARASA LA MAISHA


Watoto mapacha Maria na Consolata Mwakikuti (20) waliofariki mwishoni mwa wiki iliyoisha wataendelea kukumbukwa na mamia ya walimwengu nchini kwa kuweza kuyakubali maumbile yao waliyokuwa nayo na kujikubali mpaka kufikia hatua ya kufariki wakiwa katika mwili mmoja.

Miaka 22 iliyopita, familia ya Alfred Mwakiuki na Naomi Mshumbusi ilifanikiwa kupata watoto mapacha ambao ni Maria na Consolata lakini hawakuwa pacha wa kawaida kama jamii ya kitanzania ilivyozoea kuziona au kujaliwa nazo kwa kuwa wao walikuwa wameungana na kwa wakati huo hapakuwepo na uwezekano wa kuwatenganisha.
Akizungumza wakati wa kutoa salamu za kuaga miili ya mapacha hao Askofu Jimbo Katoliki Njombe, Alfred Maluma amesema vifo vya pacha hao vinafaa kutumiwa na watanzania kukumbushana wajibu wao kwa watu wenye ulemavu.
Mbali na Askofu Maluma, naye Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amesema mkoa wa Iringa umepata pigo kubwa la kuondokewa na pacha hao waliokuwa na upendo wa dhati na wenye kujitambua.
"Katika mkoa wa Iringa tumepata mtihani wa kuondokewa na watoto waliokuwa na upendo sana, najua kwa jinsi gani tulivyokuwa tunawapenda lakini Mungu amewapenda zaidi. Maria na Consolata walijitambua na wakakubali maumbile waliokuwa nayo halafu wakajiamini ndio maana waliweza kusoma kwa bidii na kufiki hatua ya chuo kikuu", amesema Masenza.
Pamoja na hayo, Masenza ameendelea kwa kusema "niwaombe wazazi kwamba serikali ipo tayari kuwasaidia watoto wenye ulemavu hakuna haja ya kuwaficha, waacheni watoto waje maana neema yao ipo. Kuwaficha huko ni kutenda dhambi".
Maria na Consolata walizaliwa Novemba 19, mwaka 1997 ambao enzi za uhai wao walikataa kutenganishwa miili yao na kupelekea leo hii kuzikwa kwenye jeneza moja litakalokuwa na misalaba miwili  katika makaburi ya viongozi wa dini yaliyopo Tosamaganga mkoani humo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527