KUTANA NA JAMII INAYOFUNGISHA NDOA VYURA KUVIZIA BARAKA

Wakati matukio ya kufurahisha na kusikitisha yakiripotiwa kila kukicha Duniani, huko nchini India mji wa Lagaan wananchi huwafungisha ndoa vyura kama ishara ya kuomba Baraka.

Imeelezwa kuwa wakazi wa eneo hilo huwafungisha ndoa vyura kama ishara ya kumuomba Mungu wao wa mvua awaletee Baraka za mvua katika eneo hilo ili kufanikisha shughuli zao.

Unaambiwa kuwa katika mji wa Lagaan mvua ndio kila kitu na wakazi wa eneo hilo wako tayari kufanya lolote lile ili tu kumfurahisha Mungu wao mvua.

Aidha inaelezwa kuwa katika zoezi la kuwafungisha ndoa vyura wakazi wa eneo hilo hufanya sherehe kubwa sana ambapo chura mwanaume na mwanamke huandaliwa na kupambwa vizuri kabla ya kufungishwa ndoa.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.