RAIS MAGUFULI ATEUA MAJAJI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali na Jaji Mwanaisha Athuman Kwariko kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani.

Kabla ya uteuzi huo Jaji Ferdinand Leons Katipwa Wambali alikuwa Jaji Kiongozi na Jaji Mwanaisha Athuman Kwariko alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Uteuzi huu umeanza jana Juni mosi, 2018.

Aidha, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu imesema tarehe ya kuapishwa kwa Majaji hao itatangazwa hapo baadaye.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.