MWANAJESHI WA TANZANIA AUAWA..WENGINE 7 WAJERUHIWA

Msemaji wa UN, wa New York Marekani, Stephane Dujarric
***
 Mwanajeshi wa Kitanzania aliyekuwa akilinda amani Jamhuri ya Afrika ya Kati, ameuawa baada ya kushambuliwa na maharamia wenye silaha katika kijiji cha Dilapoko, Mambere-Kadei.


Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Ofisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa, upande wa Tanzania, Stellah Vuzo leo Juni 5,2018 imesema wanajeshi wengine saba ambao wapo katika mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani(Minusca)walijeruhiwa katika shambulio hilo.


Msemaji wa UN, wa New York Marekani, Stephane Dujarric amesema wanajeshi watatu waliojeruhiwa, hali zao ni mbaya na wapo mahututi.


Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wamekemea vikali shambulio hilo linalofanywa na makundi ya watu wenye silaha na wahalifu wengine.


“Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa, linasikitishwa na kutuma salamu zao za rambirambi kwa familia ya mtunza amani huyo na linawapa pole waliojeruhiwa,” imesema taarifa hiyo


Chanzo- Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527