MOTO WATEKETEZA SOKO NA KUUA WATU 15,KUJERUHI 70 KENYA


Mfano wa picha za tukio la soko likiwa limeungua moto
****
Watu 15 wamekufa nchini Kenya kufuatia kuungua moto kwa soko lililopo jijini Nairobi, huku taarifa ikisema kwamba watu wengine 70 wamejeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Kenyatta National Hospital kwa ajili ya kupatiwa matibabu kutokana na ajali hiyo iliyokea usiku wa kuamkia leo.

Soko hilo la Gikomba ni moja kati ya masoko makubwa ya wazi nchini Kenya na mara kadhjaa limekuwa likikumbwa na ajali ya moto huku ikidhaniwa kwamba ni njama za makusudi za kuchoma moto.

Hata hivyo chanzo cha moto huo bado hakijafahamiki, baadhi ya wahanga waliteketea kwa moto na wengine kufa kutokana na kuvuta moshi wenye sumu walipokuwa wakijaribu kuokoa mali zao.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.