AZAM FC YAANIKA WACHEZAJI ITAKAOWAKOSA


Kikosi cha Azam FC kilichokuwa kinacheza katika msimu ulioisha wa ligi kuu Tanzania Bara kwa mwaka 2017/18


Ikiwa imesalia siku moja pekee kuelekea kuanza kwa michuano ya KAGAME itakayokuwa inachezewa jijini Dar es Salaam, uongozi Azam umetaja wachezaji itakaowakosa.

Kwa mujibu wa msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Idd Maganga, amesema kikosi chao kitakosa huduma ya wachezaji Tafadzwa Kutinyu, Donald Ngoma na Yakubu Mohammed.

Maganga ameeleza sababu za kukosekana kwa wachezaji Kuntinyu na Mohammed ni mapumziko ambayo waliomba wapewe hivyo watarejea siku kadhaa kabla ya ligi kuanza.

Aidha, Kocha Hans van der Plujim naye hatokuwepo kwenye benchi la ufundi la Azam wakati wa michuano hiyo kutokana na likizo yake kuwa ndefu baada ya kurejea kwao Uholanzi kwa mapumziko pia.

Mashindano hayo ya KAGAME yataanza kesho Juni 29 ambapo bingwa mtetezi Azam FC ataanza kucheza kibarua chake dhidi ya Kator FC kwenye wake wake wa nyumbani, Chamaz Complex.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527