MKE AUA MUME WAKE KISHA KUMZIKA KWA SIRI..NDUGU ALIYEKOSA MGAO WA FEDHA ATIBUA

Mwanamke mmoja nchini Uganda amekamatwa na Polisi wa nchini humo kwa kosa la kushirikina na ndugu zake kumuua mume wake na kumzika kwa siri.

Dina Ainomugisha anadaiwa kumuua mume wake ambaye alikuwa ni mfanya biashara wa ndizi kwa kile kinachodaiwa kuwa ni ugomvi juu ya mali za familia yao.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Ibanda Rogers Chebene amesema kuwa mmoja wa watuhumiwa ambaye alishiriki katika zoezi hilo ambaye hakupata mgao wake wa fedha kama walivyokubaliana ndiye aliyewapa taarifa jeshi la Polisi kuhusiana na tukio hilo.

Watuhumiwa wengine walioshiriki katika tukio hilo wametajwa kuwa ni Keresensio Mwesigye Alias Kamwesi, Experito Kacunguza, Stephen Mukama pamoja na Medrine Kabasiita ambao wote kwa sasa wametiwa nguvuni na jeshi la Polisi.

Aidha mwili wa Marehemu umechukuliwa na kupelekwa katika kituo cha Afya cha Ruhoko kwa uchunguzi zaidi.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.