MAMBA AUA MCHUNGAJI AKIBATIZA WAUMINI ZIWANI

Habari kutoka Kusini mwa Ethiopia zinasema kwamba mchungaji ambaye alikuwa akiendesha ibada ya kubatiza waumini ufukweni mwa ziwa amefariki baada ya kushambuliwa na mamba wakati akibatiza.

Mchungaji huyo ambaye ametambuliwa kwa jina la Docho Eshete alikuwa akiendesha ibada hiyo ya waumini 80 siku ya Jumapili iliyopita katika ufukwe wa Ziwa Abaya katika mji wa Arba Minch wilaya ya Merkeb Tabya.

Wakazi wa mji huo waliliambia shirika la utangazaji la BBC kwamba Mamba huyo aliruka kutoka ndani ya maji wakati mchungaji huyo akiwabatiza waumini na kumng'ata miguu,mgongo na mikono majeraha yaliyosababisha kifo chake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527