Wednesday, June 6, 2018

Picha : BASI LA HAMIDA LAGONGA TRENI NA KUUA WATU 10 KIGOMA

  Malunde       Wednesday, June 6, 2018

Watu 10 wamefariki dunia na wengine 27 wamejeruhiwa vibaya, baada ya basi la Kampuni ya Hamida kugonga treni ya mizigo mkoani Kigoma.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa polisi mkoani Kigoma Martin Otieno, amesema kwamba ajali hiyo imetokea majira ya saa 12:15 asubuhi ya leo katika eneo la Gungu, baada ya basi hilo ambalo linafanya safari zake kutoka Mkoani Kigoma kwenda Tabora, kugonga treni ya mizigo iliyokuwa ikipita kwenye njia yake, licha ya dereva wa treni kupiga honi kumpa tahadhari dereva wa basi.

Dereva wa basi hilo ambaye hajajulikana jina ni miongoni mwa watu waliofariki, huku idadi ya vifo ikitajwa kuweza kuongezeka, kutokana na majeruhi wengi kuwa kwenye hali mbaya.

Kamanda Otieno amesema kwa sasa jeshi la polisi lipo eneo la tukio likiendelea kuokoa miili na majeruhi wengine, na taarifa zingine zitafuata mara baada ya zoezi kukamilika.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post