MAWAZIRI WASIOPOKEA SIMU KUSHUGHULIKIWA

Serikali imesema iko tayari kupokea malalamiko kutoka kwa Watanzania ambao wanaona hawakutendewa haki na Mawaziri ikiwemo kutopokelewa simu zao.


Hayo yameelezwa leo Juni 26 bungeni, na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika. Mkuchika amesema simu ni sehemu ya mawasiliano.


Mkuchika ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Jaku Hashim Ayub ambaye amewashitaki mawaziri akisema kuna mawaziri wamekuwa ni tatizo kwa kutopokea simu za wabunge hivyo akasema hali inaweza kuwa mbaya kwa wananchi kama watawapigia.


Katika swali lake mbunge huyo amesema mawaziri wote wamekuwa ni tatizo kubwa katika kupokea simu za wabunge wanapowapigia na akataka namba za mawaziri ziwekwe hadharani kama ilivyo kwa namba za makamanda wa polisi wa mikoa.


“Hii ni kwa Mtanzania yeyote akiona hakutendewa haki ikiwemo simu yake kutokupokewa, aje kutoa taarifa za malalamiko na sisi tutazifanyia kazi na kama litakuwa gumu kwangu nitapeleka kwa ngazi ya juu,” amesema Mkuchika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527