BABA AMUUA MTOTO WAKE KWA PANGA KISA AMEKULA MAPARACHICHI


 Polisi nchini Kenya wanamsaka  Morris Kirema kwa kosa la kumuua mtoto wake mwenye miaka 12 na kumjeruhi mtoto wake mwingine mwenye miaka 8 kwa kutumia panga na mateke akiwashutumu watoto hao kula maparachichi kutoka katika shamba la jirani yao.

Morris anadaiwa kutumia mateke, ngumi pamoja na panga kuwaadhibu watoto hao baada ya kula maparachichi kutoka katika shamba la jirani yao na kupelekea mtoto wake huyo wa kiume mwenye miaka 12 kufa hapo hapo.

Kwa upande wa mtoto wa kike mwenye miaka 8 yeye amejeruhiwa vibaya sana pamoja na mama yake ambao wanapatiwa matibabu katika hospitali moja nchini humo.

Inadaiwa kuwa mwenye shamba ambalo watoto hao waliiba maparachichi hayo alidai alipwe kutokana na kitendo walichokifanya watoto hao na ndipo Morris alipokasirika na kunuia kuwa lazima atawaua Watoto hao wakirudi kutoka shule.

Aidha duru za kuaminika zinasema kuwa mwanaume huyo anasumbuliwa na uraibu wa michezo ya bahati nasibu na amekuwa akiwa mchungu akiombwa pesa na mke wake.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.