LIPULI FC YAONGEZA MIKATABA KWA WACHEZAJI WAKE


Mchezaji Shabani Ada (kushoto) akiwa na moja ya viongozi wa kamati ya usajili ya Lipuli FC baada ya kusaini mkataba.

Baada ya kufanikiwa kupanda Ligi Kuu msimu wa 2017/18 na kufanya vizuri ikifanikiwa kumaliza katika nafasi ya 7 kwenye msimamo, klabu ya soka ya Lipuli FC imeanza kujiimarisha kwa ajili ya msimu ujao kwa kuwaongeza mikataba wachezaji wake.

Mapema leo klabu hiyo yenye makazi yake Mjini Iringa, imewasainisha mikataba mipya wachezaji wake wanne, beki Emmanuel Kichiba, viungo Shaabani Ada, Yussuf Mohamed na mshambuliaji Malimi Busungu.

Msemaji wa Lipuli FC amesema wachezaji wote walioongezewa mikataba ni muhimu na hatua hiyo imekuja baada ya pendekezo la kocha Mkuu, Suleiman Matola kuhitaji huduma ya wachezaji hao kwa msimu ujao.

Lipuli FC imeondokewa na mchezaji wake Adam Salamba aliyekuwa tegemeo kwenye msimu uliopita ambaye amejiunga na Simba lakini Sanga amesema mipango ya kuziba nafasi hiyo inaendelea na hivi karibuni wataweka wazi.

Aidha Sanga pia amekanusha taarifa za kocha Matola kuachana na klabu hiyo huku tetesi zikisema anajiunga na mabingwa wa soka nchini klabu ya Simba ambayo nayo imeachana na kocha wake mkuu Pierre Lechantre.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.