Thursday, June 7, 2018

MAMA MBARONI KWA KUMTEKA MWANAE ILI AJIPATIE FEDHA TOKA KWA MUMEWE

  Malunde       Thursday, June 7, 2018
Mama Rose Nantongo anatuhumiwa na Polisi nchini Uganda kushirikiana na mfanyakazi wake wa zamani Edward Matovu kufeki tukio la kutekwa kwa mtoto wake Vianney Ssebulime ili ajipatie fedha kutoka kwa mume wake.

Polisi wamesema kuwa walipokuwa wakimhoji Matovu kuhusiana na utekwaji wa mtoto huyo aliiambia Polisi kuwa aliagizwa na mama wa mtoto huyo kumteka mwanae.

Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Polisi mkoa wa Kusini Lameck Kigozi amesema kuwa Matovu aliwapeleka Polisi katika kijiji cha Kananjiri nyumbani kwa Yuniya Komukama na kumkuta mtoto huyo akiwa salama.

Kwa upande mwingine John Mukisa mkazi wa kijiji cha Nabirizi alipokamatiwa Matovu amemshutumu Nantongo kwa kupenda fedha sana kuliko mwanae.

Aidha watuhumiwa hao watafunguliwa mashtaka ya utekaji wa mtoto mara tu upelelezi utakapokamilika.
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpyaHAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.bdkxfuvweev_drskoew
Previous
« Prev Post