Tanzia : MSANII SAM WA UKWELI AFARIKI DUNIA | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, June 7, 2018

Tanzia : MSANII SAM WA UKWELI AFARIKI DUNIA

  Malunde       Thursday, June 7, 2018


Msanii wa Bongo Fleva aliyetamba na vibao kadhaa ikiwemo ‘sina raha’ na ‘hata kwetu wapo’ Sam wa Ukweli amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Palestina Sinza  jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu.
Meneja na msambazaji wa nyimbo Amri the Business amesema kuwa Sam wa Ukweli amefariki majira ya saa nane usiku wa leo Alhamisi tarehe 7 Juni 2018 ambapo ni muda mfupi tu baada ya kufikishwa hospitalini hapo ambapo alikuwa anasumbuliwa na Malaria kwa muda wa wiki mbili.

Akizungumzia taarifa zilizosambaa mitandaoni kuwa marehemu alidai anaumwa ‘UKIMWI’ wa kurogwa amesema kuwa hafahamu chochote kuhusiana na taarifa hizo na ameishi na Sam kwa kipindi chote hakuwahi mshirikisha jambo hilo.

“Nimeishi na Sam kwa muda mrefu ameugua nilikuwa na taarifa za ugonjwa wake ndani ya wiki mbili lakini kuhusu suala hilo limekuwa geni na bado sijaelewa kwanini aliyezungumza kwanini amesema vile”, amesema Amri.

Amri ameongeza kuwa familia ya marehemu inaendelea na taratibu za mazishi pindi zitakapo kamilika wataweka wazi lakini taarifa za awali ni kwamba mwili utasafirishwa kupelekwa Bagamoyo kwa maziko.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post