MWALIMU MKUU AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUBAKA MWANAFUNZI UKUTANI

Mkuu wa Shule ya Sekondari Mosa Mixed, iliyopo Wilaya ya Kisasi nchini Kenya, Bwana Samuel Kimanzi (58) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kitui kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule yake.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, mtuhumiwa amepandishwa kizimbanbi leo Juni 6, 2018 na kuongeza kuwa tukio hilo la ubakaji limetokea katika shule hiyo wakati mkuu huyo wa shule alienda katika bweni la wanafunzi wa kike usiku wa Mei 21, 2018 kwa lengo la kufanya ukaguzi wa kushtukiza.

Mwanafunzi aliyebakwa alidai kwamba siku ya tukio Bwana Kimanzi, alimtoa nje ya bweni na kumpeleka katika ukuta wa shule na kisha kumbaka na kuongeza kuwa alipewa vitisho endapo angetoa taarifa za tukio hilo.

Baada ya kuripoti tukio hilo kwa wanafunzi wenzake alichukuliwa na kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa Kitui kwa matibabu ya dharura kabla ya kwenda kuripoti katika kituo cha Polisi cha Mbitini Market akiwa na walezi wake.

Kesi hiyo imetajwa kuendelea tena Septemba 3, 2018 ambapo upande wa mashtaka umepanga kuandaa mashahidi 10.

Mtuhumiwa ameachiwa kwa dhamana baada ya kukamilsha masharti ya kutoa pesa taslimu kiasi cha shilingi za Kenya 50, 000.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527