Maajabu : MAMA AJIFUNGUA MTOTO ANAYEONGEA KAMA MTU MZIMA SHINYANGA

NB- Siyo picha halisi ya mtoto katika habari

Dunia ina mambo ndivyo unaweza kusema!! Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha Nyarigongo kata ya Mwakitolyo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga 'Shinyanga Vijijini' mkoani Shinyanga amejifungua mtoto wa kiume ambaye amekuwa akizungumza wakati akiwa tumboni mwa mama yake. 

Mama wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Maria Mpago ameiambia malunde1 blog kuwa licha ya mtoto kuwa na tabia ya kuzungumza tumboni hata wakati wa ujauzito vipimo vya kitabibu vilishindwa kubaini kama ni mjamzito  licha ya kumsikia mtoto akichezacheza tumboni. 

“Nilipimwa kama nina ujauzito katika zahanati ya Mwakitolyo lakini mimba haikuonekana... nikaambiwa labda nikajaribu Kahama lakini nako haikuonekana.... basi nikaendelea kulea mimba..

....Wiki mbili zilizopita siku ya Ijumaa majira ya saa saba usiku nikasikia mtoto akiniongelesha tumboni akisema 'nipeleke msikitini nikaombewe dua,ukinipeleka  sasa mimba itaonekana,usiponipeleka itaharibika kwa kuwa mimi ni muislam ndipo kesho yake nikaenda msikitini nikakutana na shehe nikamwelezea kilichotokea akaniombea…na juzi siku ya Ijumaa Juni 1,2018 ndipo nikajifungua nyumbani”,anasimulia Maria, 

Licha ya mfululizo wa visa vya mtoto huyo ,Maria na mumewe wanasema hawana wasiwasi wowote na kwamba hali hiyo ni hali ya kawaida tu wakidai huenda ni matukio tu yanawatokea hata watu wengine. 

Mtoto huyo ambaye amewashangaza wengi anaendelea kupatiwa huduma mbalimbali za kiafya ikiwa ni pamoja na chanjo za magonjwa mbalimbali katika zahanati ya Mwakitolyo. 

Muuguzi wa zahanati hiyo Tizila Kijanda anasema hata wao wanashangazwa na visa vya mtoto huyo na kwamba wanaendelea kumpatia matibabu kama kawaida. 

Wakazi wa eneo hilo wamelihusisha tukio hilo na imani za kidini wakidai hiyo ni mipango tu mwenyezi Mungu kwani yeye ndiye muweza wa mambo yote. 
Malaki Philipo – Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527