Monday, June 4, 2018

MWALIMU ABAKA MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI BWENINI..ARUKA UKUTA

  Malunde       Monday, June 4, 2018
Jeshi la Polisi katika eneo la Laikipia nchini Kenya, linamtafuta mwalimu wa kiume ambaye anatuhumiwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la nane katika shule ya msingi Slopes View Academy.

Kwa mujibu wa Citizen Kenya imeripoti leo Juni 4, 2018 kwamba tukio hilo limetokea asubuhi ya Juni 2 ambapo mwalimu wa zamu alikutana na msichna huyo alipokuwa anaenda darasani kujisomea na ndipo alimuamuru kurudi bwenini huku akimfuata na kisha kumbaka

Mtuhumiwa wa ubakaji ambaye ni mwalimu aliruka ukuta wa shule na kukimbia baada ya kugundua taarifa za tukio hilo zimefika katika ofisi ya walimu na mama wa mwanafunzi huyo

Mwanafunzi huyo alichukuliwa na kukimbizwa katika kituo ch afya cha karibu na kupimwa ujauzito na maambukizi ya magonjwa ya zinaa bahati nzuri alikutwa yupo salama

“Tumeandika maelezo Polisi, ninachotaka ni haki kwa mwanangu, mwalimu aliyefanya hivyo akamatwe na kufikishwa mahakamani” amesema mama wa Binti

Akithibitisha tukio hilo mkuu wa Polisi katika eneo la Narumoru kamanda Job Lesikinwa amesema kwamba Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kumtafuta mtuhumiwa wa tukio hilo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post