LIONEL MESSI ALIPA KISASI KWA RONALDO


Baada ya Cristiano Ronaldo kubandikwa picha yake kubwa katika moja ya Hoteli karibu na Hoteli ambayo Lionel Messi na Argentina wamefikia, naye Messi amejibu mapigo hayo baada ya Sura yake kubandikwa katika Hoteli ambayo Argentina itakaa kabla ya mchezo wa hatua 16 bora.

Argentina ilijikuta ikifikia katika Hotelin moja ambayo pembezoni yake kulibandikwa picha kubwa ya Cristiano Ronaldo jambo ambalo lilizua mjadala mkubwa mtandaoni kuhusu namna ambayo Messi angeichukulia picha hiyo lakini baadae naye picha yake ikabandikwa katika maeneo ya Hoteli hiyo.

Argentina imefikia katika Hoteli ya Ramada katika Mji wa Kazan ambako wanajiandaa na mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya Ufaransa .

Picha ya Lionel Messi (kushoto) iliyobandikwa karibu katika Hoteli waliyofikia (kulia) Picha ya Cristiano Ronaldo iliyobandikwa karibu na Hoteli waliyofikia Argentina

Gunzo kubwa la Messi ni kuanza vibaya katika michuano ya kombe la Dunia baada ya kufungwa na Croatia katika mchezo wa ufunguzi na kutoka sare na Iceland kabla ya kuifunga Nigeria ambayo iliwapa nafasi ya kusonga mbele.

Messi amefunga goli moja pekee mpaka sasa huku Ronaldo akiwa na magoli manne katika michuano hiyo na wote wamekosa penalti moja, Messi akikosa penalty katika mchezo dhidi ya Iceland wakati Cristiano Ronaldo akikosa penalti katika mchezo dhidi ya Iran.

Kinachosubiriwa na mashabiki wa soka ni kuona wawili hao wakikutana katika michuano ya mwaka huu ya kombe la Dunia huku mpangilio ukiwa unaonesha kuwa Argentina inaweza kukutana na Ureno endapo itaifunga Ufaransa na Ureno endapo itaifunga Uruguay.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.