ATUPWA JELA MAISHA KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA MINANE


 Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 19 amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kumbaka msichana wa miaka nane.

Julius Otieno alishutumiwa kufanya kosa hilo Juni 21, 2017 katika kijiji cha Kamreri, Kaunti ya Migori nchini Kenya.

Mahakama iliambiwa kwamba Otieno alimdanganya mtoto huyo wakati akiwa njiani kutoka shuleni, akampeleka katika shamba la miwa lililokuwa karibu kisha kumbaka.

Hakimu wa mahakama ya Tongo Raymond Langat alisema mwendesha mashtaka aliweza kuthibitisha pasipo na shaka kwamba Otieno alitenda kosa hilo.

“Baada ya kuchunguza kwa uangalifu ushahidi wote na kusikia ushahidi kutoka kwa mashahidi wa pande zote na kufanya uchunguzi sahihi, mahakama imeridhika kwamba kosa lililotendeka linastahili kifungo cha maisha, “ alisema Langat
Theme images by rion819. Powered by Blogger.