Saturday, June 30, 2018

WAUGUZI WATAKIWA KUJISALIMISHA WENYEWE

  Malunde       Saturday, June 30, 2018

Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) limewataka Wauguzi wanaojijua kuwa wanatumia vyeti feki popote walipo nchini kujisalimisha mara moja kabla halijaamua kuwafuata huko waliko.


Hayo yamesemwa na Msajili wa TNMC Bi. Agnes Mtawa ambapo amebainisha kwamba katika kikao cha 193 kilichofanywa na Baraza hilo limewabaini watu 15 wanaojitambulisha kuwa ni wauguzi lakini kanzi data ya Baraza hilo imeonesha kuwa vyeti hivyo siyo halali na leseni wanazotumia ni za kugushi. 

Amesema kuwa Baraza limejadili suala la baadhi ya watu wanaogushi vyeti na leseni za taaluma ya uuguzi na ukunga ambapo limebaini kuwa katika robo mwaka Aprili - Juni, 2018 watu watano walitambuliwa kugushi vyeti na leseni hivyo wamepelekwa kwenye vyombo vya dola ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Pamoja na Baraza limewapa onyo kali Wauguzi Wakunga sita katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa kushindwa kutimiza majukumu yao ya kitaaluma wakati wakitoa huduma kwa mgonjwa hali ambayo ilipelekea mama mjamzito kupoteza mtoto kwa sababu ya uzembe.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post