AZAM FC YAFUNGA HESABU ZA USAJILI


TIMU ya Azam FC ya Dar es Salaam imetangaza kufunga hesabu za usajili kwa ajili ya msimu mpya wa mwaka 2018/19.

Wachezaji ambao mpaka sasa Azam imewasjili ni Donald Ngoma, Tafadzwa Kutinyo, Nicholas Wadada, Ditram Nchimbi na kiungo wao wa zamani Mudathir Yahya.

Meneja wa Azam FC Philip Alando amesema hawana mpango wa kuongeza wachezaji wengine kutokana na waliowasajili ndiyo walikuwa mahitaji ya benchi la ufundi.

Alisema kuwa wana mipango mizito ya kuhakikisha msimu ujao unakuwa mzuri kwao ndio maana usajili wao wameufanya mapema ili wapate muda mzuri wa kukiandaa kikosi chao kwa pamoja.

“Kwenye usajili tumeshafunga hatutaongeza wengine kilichobaki ni kujenga timu, kuwafanya hawa wapya kujenga muunganiko na wenzao waliowakuta ili waweze kucheza kitimu.

“Tunajiandaa na msimu ujao ili uwe mzuri kwetu tumepania na hakuna cha kutufanya tufikie lengo zaidi ya kujipanga mapema, tuliowasajili tunaamini wataisaidia timu kupata mafanikio,” amesema Alando.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.