JE RONALDO ATAIVUNJA REKODI YA KANE LEO??


Nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo aliyenyoosha kidole akiwa na nyota wa England, Harry Kane.

Michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi inaendelea tena leo katika viwanja vitatu ambapo nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo atakuwa dimbani kuiongoza timu yake ya taifa kukipiga dhidi ya Iran katika mchezo wa Kundi B kwenye uwanja wa Mordovia kuanzia saa 3 kamili usiku.

kuelekea mechi hiyo, Ronaldo anapewa nafasi kubwa ya kuonesha ubabe wake wa kutikisa nyavu baada ya kutikisa kamba za wapinzani mara nne katika mechi mbili alizocheza.

Endapo Ronaldo atafunga bao moja dhidi ya Iran atakuwa amemzidi nyota wa England, Harry Kane aliyefikisha mabao matano katika mashindano hayo.

Mechi nyingine zitakazopigwa ni Misri ambao wameshaaga mashindano watakamilisha ratiba dhidi ya Saudi Arabia majira ya saa 11 jioni huku pia Uruguay wakikipiga na wenyeji Urusi muda huohuo wa saa 11.
Theme images by rion819. Powered by Blogger.