"WAHITIMU NI WENGI KULIKO AJIRA,WAJIAJIRI"- NAIBU WAZIRI MAVUNDE

 Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, ajira na watu wenye ulemavu Mh. Antony Mavunde amesema kuwa Serikali inatambua kuwa wahitimu wa Elimu ya juu ni wengi kuliko mafasi za ajira.
 
Waziri Mavunde ametoa kauli hiyo bungeni leo wakati akijibu swali la Hadija Ally Mbunge viti maalum (CCM) lililohoji serikali imepanua fursa kwa kuongeza vyuo vikuu nchini, je ni kiasi gani mfuko wa vijana unaweza kuwanufaisha walengwa ikizingatiwa kuwa tatizo la ajira ni hali halisi inayowakabili vijana.

Mavunde amesema “Nafasi za ajira zinazotengenezwa kwa mwaka zimekuwa ni chache kuliko wingi wa vijana hivyob basi serikali imeanza kuwabadili mitazamo kuwa sio wote wanaoweza kukaa maofisini bali wanaweza kutumia uwezo wao na kujiajiri katika sekta za kilimo na shughuli nyingine halali zinazoweza wapatia kipato”.

Waziri mavunde ameongeza kuwa Mfuko wa Maendeleo ya vijana umeweza kufikia vikundi 397 ambapo zaidi ya Bilioni nne zimekwisha tumika kuwezesha vijana kiuchumi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527