Friday, May 18, 2018

NDUGAI AFURAHISHWA WABUNGE KUVAA KANZU NA HIJAB BUNGENI

  mtilah       Friday, May 18, 2018
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewapongeza Wabunge kwa kuvaa Kanzu kwa wingi na kwa Wabunge wa Kike kuvaa Hijab.

Spika ametoa pongezi hizo leo, Mei 18 mapema katikati ya kipindi cha maswali na Majibu kwa serikali  ambapo pia amemsifia Naibu Spika wa Bunge kwa kuvaa Baibui na Hijab.

“Wabunge kama hatujaendelea nimefanya utafiti wangu leo watu wengi sana wamependeza kwa kuvaa Kanzu na kofia hongereni sana, tukumbuke tu kanuni tunapo vaa tunatakiwa ivaliwe vilevile kama inavyovaliwa Pwani na miguu sio kuvaa kiatu cha kamba hapana unavaa kobazi,” amesema Spika Ndugai huku akicheka na Wabunge wakimpigia makofi.

“Lakini kwa upande wa kina mama leo Hijab zimekubali, lakini katika Hijab, Hijab namba moja leo hii ni ya Naibu wangu Mh. Naibu Spika, Mh. Naibu Spika ebu simama kidogo hapo ahsante sana, hiyo inaonyesha Utanzania wetu sisi ni wamoja,” ameongeza Spika.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post