Saturday, May 5, 2018

RAIS MAGUFULI AMKABIDHI MILIONI TATU MWANAFUNZI KIDATO CHA KWANZA

  Malunde       Saturday, May 5, 2018

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, mapema leo amemkabidhi mwanafunzi wa kidato cha kwanza Nundoka Msangi, kiasi cha shilingi milioni 3, kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya shule ya Sekondari Mangula mkoani Morogoro.

Tukio hilo limefanyika wilayani Mikumi mkoani Morogoro, ambapo Rais Magufuli alisimama katika kijiji cha Mangula kwa ajili ya kuongea na wananchi waliokuwa wamesimama wakati wa msafara wake akielekea Wilayani Kilombero.

Baada ya kutoa hotuba fupi, Rais Magufuli aliuliza endapo shule ya sekondari katika eneo hilo ina changamoto yoyote, ndipo kijana Nundoka akajitokeza na kusema hawana vyoo na Rais akachangia milioni tatu na kuwataka wananchi kushiriki katika ujenzi wa vyoo hivyo.
''Namkabidhi hii pesa kijana Msangi, naomba zitumike vizuri kwenye ujenzi wa vyoo na niwaombe tu wananchi mshiriki vizuri kujenga vyoo hivyo, nitarudi tena kukagua,'' amesema Rais Magufuli wakati akikabidhi fedha hizo.

Magufuli yupo Mkoani Morogoro akiendelea na ziara yake ya siku tatu ambayo inahusisha uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Baadae leo atazindua daraja la Mto Kilombero Mkoani humo.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post