MWANAMKE AINGIA KWENYE MCHEZO WA NG'OMBE KUPIGANA

Mafahali wawili wapambanapo ziumiazo ni nyasi
Mchezo wa kupiganisha ng'ombe waruhusiwa Japan baada ya karne moja
**
Mwanamke ameruhusiwa kuingia kwenye mchezo wenye asili ya utamaduni wa Japani wa kupigana na ng'ombe kwa mara ya kwanza baada ya kupigwa marufuku kwa jitihada za kuufanya mchezo kuwa wa kisasa zaidi.

Yuki Araki alimsindikiza mnyama wake katika michuano ya ufunguzi ya msimu katika kisiwa cha Hokkaido wilayani Yamakoshi.

Miaka ya hivi karibuni wanawake walipigwa marufuku wakati ambapo ulingo ulipokuwa umetakaswa na kumwagiwa mvinyo na kupakwa chumvi .

Mchezo wa Kijapani wa kupambana na ng'ombe na hatimaye kumuua ama akuue wewe unayecheza naye huitwa kwa lugha ya taifa hilo "togyu", unatofautiana na ule wa nchini Hispania ambako hairuhusiwi ng'ombe kufa.

Mchezo huu wa "togyu" wanyama hupewa mafunzo maalumu ya mchezo huo na pembe mbili za wanyama hufungana na hujaribu kwa kushinikiza kusukumana , mpaka mmoja wapo atakapo mchoma mwingine na damu kumwagika.

Kwa karne sasa nchini Japan hakukuwa na mchezo wa kupiganisha ng'ombe , mchezo maarufu wa sumo nchini humo unakabiliwa na kashfa ya ngono, wakati ambapo washiriki wanawake wa mchezo huo walipovunja ukimya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527