Wednesday, May 9, 2018

NDOTO YA HOLLYWOOD YAMTESA EBITOKE

  Malunde       Wednesday, May 9, 2018
Mchekeshaji maarufu bongo Ebitoke amesema ndoto anayoiota ya kuja kukanyaga ardhi ya Hollywood siku moja, ana imani itatimia na iwapo atakufa bila kutimia basi atakufa bila kuwa na amani.

Akiwa KIKAANGONI East Africa Television, Ebitoke amesema kwamba ndoto yake kubwa siku moja ni kuigiza filamu za Hollywood na kufanya kazi na wasanii wa Hollywood, na hata watu wakitaja Hollywood wawe wanaitaja na Tanzania.

Ndoto yangu ni kufika Hollywood, nikifa bila kutimiza hiyo ndoto, sidhani kama nitaenda kwa amani, nataka watu watakapotaja Hollywood waitaje na Tanzania, Mimi nataka niwe hata zaidi ya Lupita Nyong'o, yaani nikilala nikiamka naiota Oscar hii hapa, na mpaka niipate”, amesema Ebitoke

Ebitoke ameendelea kwa kusema kwamba hata filamu yake ambayo ameigiza akisubiri kuitoa ina viwango vya kimataifa, na wana malengo ya kuiingiza kwenye tuzo za kimtaifa ili iweze kufika Hollywood.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post