Friday, May 4, 2018

MTOTO AKUTWA NA SINDANO 7 ZA KUSHONEA NGUO TUMBONI

  Malunde       Friday, May 4, 2018
Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu mkazi wa kijiji cha Keringet kaunti ya Pokot amekutwa na sindano 7 za kushonea kwa mkono tumboni mwake, baada ya kupigwa picha ya xray.


Mtoto huyo alipelekwa hospitali ya Kapenguria siku ya Jumanne kupata matibabu ya maumivu ya tumbo ambayo alikuwa akiyapata kwa muda mrefu bila kujua tatizo ni nini.

Bibi yake Bi. Emily Linga'a ambaye ndiye anayeishi naye, amesema mtoto huyo alikuwa akilalamika maumivu ya tumbo kwa zaidi ya miaka miwili, lakini hawakuweza kubaini mara moja chanzo cha maumivu hayo na kuendelea kumpatia dawa za kutuliza maumivu, lakini baada ya kuona anazidi kualalamika walimpeleka hospitali na kugundua ana tatizo hilo.

“Kwanza nilidhani mtoto alikuwa na minyoo, sikuwahi kufikiria kwamba ana sindano tumboni mwake, nilikuwa nahisi ni malaria siku zote na kumpa dawa za maumivu”, amesema bibi huyo ambaye anaishi naye, baada ya mama yake kumuacha alipoolewa na mwanaume mwengine.

Madaktari wa hospitali hiyo wamempa rufaa ya kwenda hospitali kubwa ya Moi ili kuweza kufanyiwa upasuaji wa tumbo, na kutolewa sindano hizo ambazo hazijajulikana zimeingiaje.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post