Friday, May 4, 2018

MAHAKAMA YAZUIA KWA MUDA MATUMIZI YA KANUNI ZA MTANDAO

  Malunde       Friday, May 4, 2018
Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara leo Mei 4, 2018 imetoa zuio la muda linalozuia matumizi ya Kanuni za Maudhui ya Kimtandao ambazo matumizi yake yalipaswa kuanza rasmi Mei 5, 2018.

Katibu wa Jukwaa la Wahariri (Tef), Neville Meena amesema zuio hilo limetolewa leo baada ya taasisi sita, ikiwemo Tef, kuwasilisha mahakamani maombi ya kuzia matumizi ya kanuni hizo April 30, 2018.

Taasisi zilizowasilisha maombi hayo mahakamani ni Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (LHRC), Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRD), Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jamii Media, Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa) na Tef.

Taasisi hizo katika kesi ya msingi ya mapatio ya kanuni hizo, zimewashitaki Waziri wa Habari, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katika maombi ya msingi taasisi hizo zinaiomba Mahakama Kuu kufanya mapitio ya kanuni hizo kwa kigezo kwamba; Waziri ametumia nguvu ya kisheria nje ya mamlaka yake, zinakiuka kanuni za usawa, kanuni hizo zinapingana na haki ya kujieleza, haki ya kusikilizwa pamoja na haki ya usiri.

Kesi ya msingi imepangwa kusikilizwa Mei 10, 2018.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post