MKUU WA WILAYA ATAKA UCHUNGUZI UFANYIKE TUHUMA ZA MWALIMU KUNAJISI WANAFUNZI DAR

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Salum Hapi ameliagiza Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tuhuma za mwalimu wa kiume katika Shule ya St Florence ya jijini Dar es Salaam kudaiwa kuwanajisi wanafunzi.


Ameagiza kutafutwa na kukamatwa kwa mwalimu huyo anayetuhumiwa kufanya vitendo hivyo ambaye tangu Machi 16, 2018 haonekani shuleni hapo.

Tangu jana jioni kumekuwa na taarifa za mwalimu mmoja wa shule hiyo kuwanajisi watoto wanne wa darasa la saba, jambo lililozua taharuki.

Mkuu huyo wa wilaya alipowasili shuleni hapo alipokewa na mwalimu mkuu, Wilson Mwabuka huku baadhi ya walimu wakitimua mbio na kujifungia wakihofia kupigwa picha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post