WATUMIAJI WA FACEBOOK NA WHATSAPP KULIPA KODI UGANDA...RAIS HATAKI UDAKU

Museveni alisisitiza kuwa ya kijamii inapaswa kulipa kodi kwasababu inachochea taarifa za udaku

Raia wa Uganda wanaotumia mitandao ya kijamii nchini humo huenda wakalazimika kulipa ndipo waruhusiwe na serikali kutumia mitandao ya kijamii kama vile Facebook na WhatsApp.

Hii ni baada ya Bunge hilo kuidhinisha mswada huo tata Jumatano.

Chini ya sheria hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kutekelezwa 1 Julai, wanaotumia mitandao ya kijamii watakuwa wanatozwa shilingi 200 za Uganda ambazo ni sawa na $0.05 ( £0.04) kila siku.

Raia pia watalipia kila shughuli ya kibiashara watakayoikamilisha kupitia simu zao, huku kila shughuli ya kibiashara ikitozwa 1% ya thamani yake.

Rais Yoweri Museveni alikaririwa na vyombo vya habari nchini Uganda mwezi uliopita akisema kuwa mitandao ya kijamii inatumiwa zaidi kwa taarifa za "udaku".

Wanaharakati wa haki za binadamu hawakubaliani na madai ya rais.

"Ni sehemu tu ya majaribio ya kubana uhuru wa watu kujieleza ," Mwana Blogi Rosebell kagumile aliliambia shirika la habari la Reuters.

Takriban wabunge watatu wamekosoa sheria hizi mpya na kuzitaja kama "utozaji wa kodi mara dufu ", kulinga na gazeti binafsi Daily Monitor.

Mbunge wa jimbo Kyaddondo Mashariki Robert Kyaggulanyi, almaarufu Bobi Wine - pamoja na wenzake Joshua Anywarach na Silas Aogon - wamesema kwa sababu watumiaji wa mtandao wa WhatsApp hupata huduma hiyo kupitia muda salio ambalo wanalipia ushuru, ushuru wa ziada utakuwa unakiuka haki

Mbunge mwingine , Patrick Nsamba wa chama tawala , amesema kuwa ushuru huo utawaumiza maskini zaidi

Ni rahisi sana kwa mbunge kusema asilimia 1% ni kiasi kidogo cha lakini kwa watu wenye kipato cha chini ya dola moja kwa siku itawaumiza sana

Kuna mkanganyiko kuhusu namna ushuru huo mpya kwa mitandao ya kijamii utakavyotekelezwa.Mbunge wa jimbo Kyaddondo Mashariki Robert Kyaggulanyi, almaarufu Bobi Wine ni mmoja wa watu wanaopinga sheria ya kodi kwa matumizi ya mitandao ya kijamii

Waganda wanatumia mitandao ya kijamii kusambaza kauli zao za kutoafikiana na ushuru huo mpya ambao umepitishwa kufuatia ombi la rais Yoweri Museveni.

Katika barua yake kwa waziri wa fedha, Bwn. Museveni alisisitiza kuwa ya kijamii inapaswa kulipa kodi kwasababu inachochea taarifa za udaku.

Lakini alidai kuwa huduma ya data za intaneti haipaswi kuwekewa ushuru, kwa sababu manufaa yake ya kielimu.

Wataalam pamoja na mtoaji mmoja wa huduma za Intaneti wameelezea hofu yao juu ya namna ushuru wa mitandao ya kijamii na mamilioni ya Waganda kwa kutumia sim-kadi

Serikali inahangai kuhakikisha simu kai zote zinasajiliwa.

Mitandao ya kijamii imekuwa nyenzo muhimu ya kisiasa nchini Uganda kwa chama tawala na upinzani.

Huduma ya mitandao hiyo ilifungwa wakati wa uchaguzi wa 2016.
Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post