Wednesday, May 30, 2018

KATIBU MKUU MPYA WA CCM APOKELEWA KWA SHANGWE UDSM

  Malunde       Wednesday, May 30, 2018
Katibu Mkuu Mteule wa CCM Dk Dk Bashiru Ally akizungumza na Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dk Rasul Ahmed Minja alipowasili chuoni hapo. 

Katibu Mkuu Mteule wa CCM, Dk Bashiru Ali amewasili katika viunga vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alikokuwa akifundisha.

Dk Bashiru ameonekana leo Mei 30, katika chuo hicho, akisalimiana na kupongezwa na wahadhiri wenzake pamoja na wanafunzi, ikiwa ni siku moja baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo.


Dk Bashiru ametuliwa jana na Halmashauri Kuu ya CCM, kushika nafasi hiyo, akimrithi Abdulahman Kinana.


Awali baada ya kiongozi huyo kufika chuoni aliingia katika jengo la Utawala na baadaye kuelekea Idara ya Sayansi ya Sanaa na Utawala alikokuwa akifanyia kazi.


Akiwa kwenye idara hiyo, Dk Bashiru alizungumza na Mkuu wa Idara hiyo, Rasul Ahmed Minja ambaye pia alimlaki kwa shangwe na kumpongeza kwa uteuzi.


Na Tumaini Msowoya, Mwananchi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post