Utafiti : JOTO HUCHANGIA WATU KUFELI MITIHANI SHULENI

Kiyoyozi husaidia sana wakati hali ya hewa inapokuwa ya joto

Utafiti uliofanywa n watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Harvard na vyuo vingine vikuu vya Marekani kuna uhusiano wa "kuaminika" kati ya viwango vya juu vya joto na mafanikio ya shuleni.

Vipimo vya uchanganuzi wa alama miongoni mwa wanafunzi wa shule za sekondari milioni 10 vilivyochukuliwa katika kipindi cha miaka 13 ya joto vinaonyesha kuwa majira ya joto yana athari hasi kwa matokeo ya shule.

Utafiti huo unasema labda njia ya kukabiliana na athari hiyo inaweza kuwa ni kutumia viyoyozi zaidi.

Wanafunzi wanaofanya mitihani wakati wa majira ya joto wamekuwa wakilalamika kuwa wanasumbuliwa na joto.

Lakini utafiti huu kutoka kwa wasomi wa Chuo Kikuu cha Harvard, Chuo kikuu cha California Los Angeles (UCLA) na kile cha kitaifa cha Georgia wanadai kuwa wamepata ushahidi wa wazi unaoonyesha kwamba wakati kunapokuwa na joto matokeo ya mitihani ya shule hushuka.Watu wengi wanaoishi maeneo ya joto hujimwagia maji baridi kupoza mwili
Wimbi la joto

Utafiti uliochapishwa na taasisi ya uchunguzi wa kiuchumi nchini Marekani, ulibaini kuwa wanafunzi walikuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa na alama za chini wakati wa miaka ya joto na matokeo mazuri wakati wa miaka yenye vipindi vya baridi.

Matokeo haya yalikuwa sawia katika maeneo yenye tabia nchi tofauti - iwe ni kwa majimbo yenye baridi zaidi ya kaskazini mwa Marekani au majimbo yenye vipimo vya juu vya joto ya kusini mwa Marekani, joto lilionekana kuathiri matokeo ya mitihani shuleni.

Utafiti huo kuhusu Joto na Masomo, unasema kwamba hali ya hewa ya joto huwafanya wanafunzi washindwe kujifunza na kuwa makini wanapofanya kazi wanazopewa shule wazifanyie nyumbani.,

Utafiti huo umebaini pia kuwepo kwa athari za hali ya hewa ya joto katika uchumi wa familia zenye kipato cha chini na wanafunzi wanaotoka katika jamii za walio wachache.

Kulikuwa na madai kwamba familia tajiri zaidi na shule katika maeneo ya watu wenye kipato cha chini waliweza kuingilia kati pale walipoona watoto wanalala darasani na kutafuta muda mbadala wa kuwapatia masomo ya ziada baada ya shule.
Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527