Friday, May 4, 2018

VINARA WA RUSHWA MKOANI SHINYANGA WAANIKWA

  Malunde       Friday, May 4, 2018
Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga, Gasto Mkono akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 4,2018 ofisini kwake-Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
****
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Shinyanga imezitaja idara zinazoongozwa kwa kulalamikiwa kwa vitendo vya rushwa kuwa ni serikali za mitaa, sekta binafsi ,mahakama,polisi,elimu na ardhi.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo,Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga, Gasto Mkono alisema katika kipindi cha Julai 2017 hadi Machi 2018 wamepokea taarifa 181 za vitendo vya rushwa huku serikali za mitaa,sekta binafsi,mahakama na polisi wakiongoza kwa kulalamikiwa.

“Kati ya taarifa 181 tulizopokea baadhi yake zimefanyiwa kazi na kazi imekamilika na zingine zinaendelea kufanyiwa uchunguzi,idara zilizolalamikiwa zaidi ni serikali za mitaa ambapo kuna taarifaa 65, sekta binafsi (37),mahakama (20),polisi (13),elimu (13),ardhi (9),siasa (7),afya (5), TRA (4),mifuko ya hifadhi ya jamii (4) na uhamiaji (4)”,alifafanua Mkono.

Hata hivyo alisema mbali na idara hizo kulalamikiwa kuwa vinara wa vitendo vya rushwa haimaanishi kuwa katika idara ama sekta zingine hakuna vitendo vya rushwa hivyo kuwataka wananchi kutoa taarifa pale wanapobaini kuwepo kwa vitendo vya rushwa.

Alisema hivi sasa kesi zinazoendelea mahakamani ni 19 zikiwemo kesi mpya 13 zilizofunguliwa katika kipindi cha mwezi Julai 2017 hadi Machi 2018.

“Kwa upande wa fedha za SHIRECU hadi kazi hii itakapokamilika tunatarajia kuokoa zaidi ya shilingi milioni 200 ambazo zilifanyiwa ubadhilifu katika vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) kwa msimu wa mwaka 2012 hadi mwaka 2016,zitarejeshwa kwa wana Ushirika wa SHIRECU na wahusika kufikishwa mahakamani”,aliongeza Mkono.

Katika hatua nyingine alisema TAKUKURU inaendelea kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika halmashauri za wilaya na kuangalia thamani ya fedha zilizotumika kwa kulinganisha na miradi yenyewe ilivyotekelezwa.

Na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga, Gasto Mkono akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake -Picha na Kadama  Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga, Gasto Mkono akizungumza na waandishi wa habari
Waandishi wa habari wakichukua dondoo muhimu
Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga, Gasto Mkono akizungumza na waandishi wa habari.
Picha na Kadama  Malunde - Malunde1 blog

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post