Friday, May 4, 2018

RAIS MAGUFULI : NAFUU ULE SUMU BADALA YA KULA HELA ZA SERIKALI

  Malunde       Friday, May 4, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amesema kwamba watu wanaokula fedha za serikali wanajitafutia balaa, kwani ni sawa na wanakunywa sumu.


Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Morogoro alipokuwa akizindua ujenzi wa babara ya ya Kidatu - Ifakara , na kueleza kwamba wakandarasi hao waliokula hela za miradi wamekunywa sumu, hivyo wajiandae kuhukumiwa au kurudisha fedha hizo.

“Kuna baadhi ya miradi makandarasi wamekula pesa, nataka kuwahakikishia hao wakandarasi wamekula sumu, hela za serikali haziliwi, ni nafuu ukale sumu kuliko kula hela za serikali ya awamu ya tano, Na mimi nataka niwaeleze ukweli kama wapo hapa makandarasi, wamekula sumu tena ile sumu kali, nimeagiza wakandarasi wote waliopewa miradi ya maji, waanze kuishughulikia, au wajiandae kuhukumiwa, au wajiandae kurudisha hizo fedha”, amesema Rais Magufuli.

Sambamba na hilo Rais Magufuli amewataka wakandarasi wa miradi ya barabara ya hiyo mkoani Morogoro kukamilisha miradi hiyo kwa wakati, ili wananchi waweze kuitumia.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post