Saturday, May 5, 2018

FAMILIA YA HECHE KUWEKA WAKILI KUSIMAMIA KESI YA MAUAJI YA SAGUTA

  Malunde       Saturday, May 5, 2018
Baada ya maziko ya Suguta Chacha (27) aliyeuawa kwa madai ya kuchomwa kisu akiwa mikononi mwa polisi katika kituo cha Sirari, wilayani Tarime familia yake imesema itaweka wakili kusimamia kesi ya ndugu yao mahakamani.


Suguta ambaye ni ndugu wa mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema),John Heche anadaiwa kuuawa kwa kuchomwa kisu na polisi usiku wa kuamkia Aprili 27.


Heche amesema kwamba ndugu yao alifanyiwa kitendo cha kinyama na kubainisha kuwa wataweka wakili ili mtuhumiwa wa mauaji hayo apate hukumu anayostahili.


“Tunajua yupo wakili wa jamhuri atakayesimamia kesi, lakini nasi tutaweka wetu, tunachotaka ni kwa aliyehusika kupata hukumu anayostahili, familia imeshajipanga kwa ajili ya jambo hilo,” alisema Heche.


Alisema kiuhalisia hakuna fidia yoyote wanayoweza kulipwa ikazidi uhai wa ndugu yao, isipokuwa ni kwa mhusika kuchukuliwa hatua za kisheria.


“Tunamshukuru Mungu tumemzika salama, hakuna jambo lolote la kushtua lililojitokeza wakati wa shughuli nzima ya kumuhifadhi ndugu yetu. “Watu walijaa, huzuni na simanzi viliutawala msiba huu ambao unatuumiza sana,” alisema Heche.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post